WALIMA Zabibu kutoka makao makuu ya Tanzania, Dodoma Jiji wamefikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba wa Masoud Djuma ambaye alikuwa ni kocha mkuu.
Mbali na Djuma ni benchi lote la ufundi la timu hiyo limevunjwa kwa ajili ya kufanya maboresho upya.
Ni Mohamed Muya huyu alikuwa ni kocha msaidizi ndani ya Dodoma Jiji ambayo ilikuwa kwenye mwendo wa kusuasua.
Taarifa iliyotolewa na Dodoma Jiji imeeleza kuwa ni Omary Omary atakuwa kocha wa muda kwenye timu hiyo kwa sasa.
Mchezo wa mwisho wa Djuma kukaa kwenye benchi ilikuwa dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ni mabao 3-0 alikubali kupoteza pointi tatu ugenini baada ya mchezo uliopita kushinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold.
Djuma aliweka wazi kuwa bado alikuwa anatengeneza kikosi hicho na imani yake ilikuwa kupata matokeo kwenye mechi zijazo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE