Home KIMATAIFA EMERY ATUA ASTON VILLA KURITHI MIKOBA YA GERRARD

EMERY ATUA ASTON VILLA KURITHI MIKOBA YA GERRARD

0

Klabu ya Aston Villa imemchukua Meneja wa zamani wa Arsenal Unai Emery (50) kuiongoza klabu hiyo baada ya Steven Gerrard kufukuzwa kazi.

Gerrad alifukuzwa wiki iliyopita baada ya mechi dhidi ya Fulham ambapo Villa ilifungwa 3-0.

Kocha huyo ataanza kazi mwezi ujao baada ya kukamilisha vibali vya kufanyia kazi.

Dili hilo tayari limekamilika na kesho Jumanne Oktoba 25 atafanya mkutano wa kuwaaga Villarreal.

Alijiunga na Villarreal mwaka 2020 na kuwapa mafanikio katika ligi ya Uropa.

Lakini pia aliwafikisha mara mbili katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here