Home KIMATAIFA GREENWOOD NA MANCHESTER UNITED AFIKISHWA MAHAKAMANI, KESI YAKE YAAHIRISHWA

GREENWOOD NA MANCHESTER UNITED AFIKISHWA MAHAKAMANI, KESI YAKE YAAHIRISHWA

0

Mchezaji wa Manchester United Mason Greenwood amefikishwa mahakamani kwa makosa ya ubakaji, kushambulia na utekaji.

Baadhi ya jamaa na wanafamilia wa mchezaji huyo wa Manchester United walikuwepo mahakamani hapo huku Greenwood akiwa amevalia shati la kijivu na viatu vya kufanyia mazoezi.

Mchezaji huyo anakabiliwa na mashitaka matatu yote yanamuhusu mwanamke mmoja.

Greenwood, 21, alikamatwa mnamo Januari mwaka huu na kuchiwa kwa dhamana. Lakini alikamatwa tena siku ya Jumamosi kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana hiyo.

Akiwa mahakamani hapo, Greenwood alithibitisha jina lake, tarehe ya kuzaliwa na anwani yake ya makazi wakati kesi yake ilipokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Hakimu wa Manchester.

Maelezo ya mashitaka ya mchezaji huyo yalisomwa kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo na baada ya hapo taratibu za dhamana zitaamuliwa.

Inasemekana alifanya jaribio hilo la ubakaji Oktoba 2021. Pia alifanya shambulio la mwili mnamo Desemba 2021, na kumweka katika himaya yake kinguvu mwanamke huyo kati ya Novemba 2018 na Oktoba mwaka huu.

Manchester United ilimsimamisha Greenwood wakati tuhuma hizo zilipoibuka na hajacheza wala kufanya mazoezi na klabu hiyo tangu wakati huo.

Ameifungia United mara 35 katika mechi 129.

Greenwood pia aliondolewa kwenye mchezo maarufu wa video wa FIFA 22 na Nike ikasitisha mkataba wake wa udhamini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here