Home KIMATAIFA HAG AWATUPIA VIJEMBE RONALDO, DE GEA NA RASHFORD

HAG AWATUPIA VIJEMBE RONALDO, DE GEA NA RASHFORD

0

Kocha wa Manchester United amewataka wachezaji ambao mikataba yao ipo ukingoni kumalizika kuacha kufikiria habari ya mikataba mipya na badala yake waendelee kujituma uwanjani.

Amesema ni vema wachezaji ambao mikataba yao ipo ukingoni ni vema waweke akili yao katika kuisaidia timu badala ya kuanza kuvurugwa.

Cristiano Ronaldo , Davide de Gea na Marcus Rashford ni miongoni kwa wachezaji ambao mikataba yao inaisha mwisho wa msimu.

Hata hivyo, nyota hao ambao walicheza katika mechi ya Jumapili ambayo United imetoka sare na Newcastle, bado wana kipengele cha kuongeza mwaka mmoja katika mikataba yao.

” Kwa kipindi hiki, tunaangalia zaidi kujituma uwanjani na sio minong’ono au mazungumzo ya mikataba,” amesema.

” Bado tuna mechi nyingi sana mbele yetu, sio wakati wa kuanza kujadili mazungumzo au minong’ono,” ameongeza.

Amesema United inahitaji wachezaji wanaojituma na kwa bahati nzuri ndio aina ya wachezaji alionao kwa sasa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here