Home KIMATAIFA HAWA HAPA WATUPIAJI KIMATAIFA

HAWA HAPA WATUPIAJI KIMATAIFA

0

KWENYE anga la kimataifa rekodi zinaonyesha kuwa namba za wazawa kufurukuta ni finyu kutokana na wageni kutawala kila kona.

Yanga na Simba wanaperusha bendera kwenye Ligi ya Mabingwa huku Azam FC kwenye Kombe la Shirikisho wao mchezo wao walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Al Akhadar ya Libya wana kazi ya kufanya mchezo wa marudio.

Kwenye mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo Yanga imecheza imekusanya jumla ya mabao 10, ilianza kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Zalan FC na ule wa pili ilishinda mabao 5-0 dhidi ya Zalan.

Mchezo wa tatu hatua ya raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika ilianza kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Al Hilal.

Hapa tunakuletea orodha ya watupiaji wa mabao ambapo kila timu vinara ni wageni jambo linapaswa kuwapa hasira wazawa namna hii:-

Fiston Mayele

Alianza kwaZalan FC aliwatungua mabao 6 kwenye mechi mbili na aliwatungua bao moja Al Hilal.

Mayele ni namba moja kwa wenye mabao mengi katika hatua hii akiwa ni raia wa DR Congo mzee wa kutetema.

Mabao yote kayafunga kipindi cha pili ambapo dhidi ya Zalan FC alifunga dakika ya 45,85 na 88 kwenye mchezo wa kwanza na alitoa pasi moja ya bao kwa Feisal Salum dakika ya 55.

Kwenye mchezo wa pili, Mayele alifunga mabao matatu dhidi ya Zalan dakika ya 59,62 na 66 kwa pasi ya Jesus Moloko raia wa dr Congo  na lile dhidi ya Al Hilal alifunga dakika ya 50 kwa pasi ya Khalid Aucho raia wa Uganda.

Katika mabao 10 kimataifa kahusika kwenye 8 hivyo inaonyesha kuwa mfumo wa Yanga huyu ni mtengeneza mipango namba moja.

Aziz KI

Kiungo Aziz KI wa Burkina Faso yeye ametupia bao moja ilikuwa dhidi ya Zalan FC mchezo wa pili wakati ikishinda mabao 5-0, alifunga bao hilo dakika ya 85.

Feisal Salum

Kiungo huyu mzawa mkali wa mashuti yenye ujazo kwenye mguu wake wa kulia katupia bao moja na kutengeneza pasi moja alimpa Farid Mussa, alifunga kwenye mchezo dhidi ya Zalan FC kwenye ushindi wa mabao 4-0 dakika ya 55

Farid Mussa

Mzawa huyu alifunga bao moja dhidi ya Zalan FC wakati Yanga ikishinda mabao 5-0 kwa pasi ya Feisal Salum.

Simba

Watani zao wa jadi Simba walianza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Big Bullets na mchezo wa pili walishinda mabao 2-0 dhidi ya Big Bullets.

Katika hatua ya raundi ya Pili Simba imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya de Agosto ya Angola.

Moses Phiri

Phiri raia wa Zambia ana mabao manne kimataifa.Alifunga bao moja dhidi ya Big Bullets ugenini kwa pasi ya Kibu Dennis na alifunga mabao mawili Uwanja wa Mkapa dhidi ya Big Bullets kwa pasi ya Clatous Chama na moja alifunga kwa pasi ya Agustino Okra raia wa Ghana.

Clatous Chama

Chama raia wa Zambia mwenye pasi tatu kimataifa alifunga bao moja dhidi ya de Agosto kwa pasi ya Okra ugenini.

John Bocco

Nahodha mzawa Bocco ana bao moja kimataifa alifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Big Bullets akitumia pasi ya Chama.

Israel Mwenda

Beki pekee mwenye bao kimataifa ni Israel Mwenda ambaye ni mzawa alifunga bao hilo dhidi ya de Agosto akitumia pasi ya kiungo wa kazi ngumu Sadio Kanoute.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here