Home KITAIFA HAYA NI MATUKIO YA SOKA YALIYOONDOA ROHO ZA WATU DUNIANI

HAYA NI MATUKIO YA SOKA YALIYOONDOA ROHO ZA WATU DUNIANI

0

Baada ya watu 174 kufariki na 180 kujeruhiwa nchini Indonesia, Jumapili, Oktoba 2, 2022 wakati wa mechi ya East Java involving Arema FC na Persebaya Surabaya huko Java Mashariki, matukio mengine ndani ya miaka 40 iliyopita ni:

Januari 2022, Cameroon Watu nane walipoteza maisha na watu 38 wakijeruhiwa katika Dimba la Yaounde Olembe nchini Cameroon.

Februari 2012, Misri Mashabiki 73 walifariki dunia na wengine zaidi 1,000 kujeruhiwa wakati wa mechi kati ya Al-Masry na Al-Ahly katika Jiji la Port Said. Ligi Kuu ya Misri ilisimamishwa kwa miaka miwili.

Machi 2009, Ivory Coast Watu 19 waliuawa Abidjan katika Dimba la Felix Houphouet-Boigny kabla ya kuanza kwa mechi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia dhidi ya Malawi.

Mei 2001, Ghana Takribani watu 126 waliangamia katika Dimba la Accra wakati polisi waliporusha mabomu ya machozi kufuatia vurugu za mashabiki.

Aprili 2001, Afrika Kusini Watu 43 walipoteza maisha wakati wakilazimisha kuingia katika Dimba la Ellis Park, Johannesburg.

Oktoba 1996, Guatemala Watu 82 walipoteza maisha na wengine 147 walijeruhiwa kufuatia ugomvi wa mashabiki wakati wa mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia baina ya Guatemala na Costa Rica katika Jiji la Guatemala City.

Mei 1992, Ufaransa Dimba la Bastia Furiani liliaguka na kuua watu 18 na kujeruhi watu 2,300 wakati wa mechi ya nusu fainali kati ya Bastia na Olympique de Marseille. Bunge la Ufaransa lilipitisha sheria mwaka jana kuwa hakuna mechi yoyote itakayochezwa nchini humo Mei 5, hii ikiwa ni sehemu ya heshima na kuwakumbuka waathirika wa tukio hilo.

Januari 1991, Afrika Kusini Watu 42 walifariki dunia wakati wa mechi ya maandalizi ya msimu (pre-season) katika Dimba la Oppenheimer huko Orkney kwenye mechi ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates. Mashabiki wa Orlando waliwavamia mashabiki wa kaizer na kuwachoma visu.

Aprili 1989, Uingereza Watu 96 ambao ni mashabiki wa Liverpool walipoteza maisha baada ya jukwaa la uwanja kuanguka na kuwafunika mashabiki hao waliokuwa wamesongamana katika Dimba la Hillsborough huko Sheffield kabla ya mechi ya nusu fainali Kombe la Shirikisho la Uingereza (FA Cup) kati ya Liverpool na Nottingham Forest.

Mwathirika mwingine amefariki dunia hivi karibuni, Juni, ikiwa ni miaka takribani 32 akiugua tatizo la ubongo kutokana na ajali hiyo.

Machi 1988, Nepal Katika Dimba la Taifa la Nepal, huko Kathmandu, zaidi ya mashabiki 90 walipoteza maisha kufuatia mlango wa kutokea kufungwa na kusababisha msongamano mkubwa.

Mei 1985, Ubelgiji Watu 39 walipoteza maisha na wengine zaidi ya 600 wakijeruhiwa kutokana na vurugu zilizoibuka wakati wa mechi ya fainali ya European Cup kati ya Juventus na Liverpool kwenye Dimba la Heysel Brussels.

Mei 1985, Uingereza Takribani watu 56 walifariki na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa wakati wa mlipuko katika Dimba la Valley Parade huko Bradford kwenye mechi ya ligi daraja la tatu dhidi ya Lincoln City.

Oktoa 1982, Urusi Mashabiki zaidi ya 66 walipoteza maisha kufuatia shambulio wakati wa mechi ya UEFA Cup kati ya Moscow na Dutch kwenye Dimba la Luzhniki Stadium, huko HFC Haarlem, Moscow.

Maofisa wa Serikali hiyo ya Kisovieti hawakuwahi kueleza kwa miaka mingi kuhusu undani wa tukio hilo n ahata idadi halisi ya watu waliopoteza maisha huku ikitajwa kuwa idadi hiyo inafikia watu 340.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here