Home KITAIFA HESABU ZA AZAM FC KIMATAIFA HIZI HAPA

HESABU ZA AZAM FC KIMATAIFA HIZI HAPA

0

KALLY Ongala, kocha wa washambuliaji wa Azam FC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa dhidi ya Al Khadar ya Libya.


Azam FC imewasili nchini Libya ikiwa na msafara wa wachezaji 25 miongoni mwao ni washambuliaji wawili, Idris Mbombo na Prince Dube.


Pia kiungo Abdul Suleiman, ‘Sopu’ ni miongoni mwa waliopo kwenye orodha ya mastaa wa Azam FC itakayoshuka kesho kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.


Ongala amesema:”Tunatambua kwamba tuna kazi ngumu kimataifa na lengo ni kupata ushindi hilo linawezekana.


“Ushindi wa ugenini utaongeza kasi yetu ya kuweza kupata ushindi kwenye mechi yetu ya marudiano,” .

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here