Katika pambano lililopigwa jana Bondia Mtanzania Ibra Class amefanikiwa kumchapa bondia Alan Pina kutoka nchini Mexico kwenye Pambano la raundi 12 ambalo halikuwa la ubingwa lililofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.
Tangu Mwanzo wa pambano hilo Pina alionyesha upinzani mkali kwa Ibrahimu Class mpaka ilipofika raundi ya 9 ambapo Alan Pina alipigwa ngumi mbili nzito ambazo zilimpelekea kwenda chini na kudaiwa kupoteza fahamu na hivyo kulazimika kupewa huduma ya haraka ili kunusuru maisha yake.
Aidha, kutokana na ushindi huo Tanzania inaendelea kuandika rekodi mpya katika mchezo wa dondi baada ya mabondia wake wengi kuendelea kufanya vizuri katika mapambano mbalimbali ya ndani pamoja na yale ya kimataifa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE