Home KITAIFA IHEFU FC YAIPA KICHAPO DODOMA JIJI

IHEFU FC YAIPA KICHAPO DODOMA JIJI

0

DAKIKA 540 ambazo ni mechi sita, Ihefu ilicheza bila kuambulia ushindi ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha mpya Melis Medo aliyechukua mikoba ya Masoud Djuma.

Uwanja wao wa nyumbani wa Highland Estate ulichezwa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ni mabao ya Jaffary Kibaya dakika ya 22 na Obrey Chirwa dakika ya 33 yalitosha kuipa ushindi Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mwambusi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here