WAKATI mwingine furaha huwa inabebwa na maumivu jambo ambalo linafanya maisha yaendelee kuwa maisha hakuna namna ni hali halisi ilivyo.
Ikiwa upo kwenye mazingira mazuri basi huo uzuri acha uendelee kunogeshwa na yale ambayo yatatokea ndani ya Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Simba.
Hakika unatarajiwa kuwa mchezo mgumu na wenye ushindani kwa kila timu lakini ukweli ni kwamba atakayepata matokeo mazuri ni hongera kwake na atakayekosa matokeo mazuri anajukumu la kujipanga upya.
Hakuna namna dakika 90 ni muda mzuri wa kutoa majibu ya kile ambacho kinahitajika kwa kila timu hivyo kwa muda ambao mlikuwa mkifanya maandalizi nina amini kwamba kila kitu kitakuwa kipo kwenye mstari.
Mechi hii ni kubwa na dunia nzima kwenye ulimwengu wa mpira inafuatilia hivyo wachezaji wakati mwingine wa kuendelea kufuata sheria 17 za mpira ili kupata kile ambacho mnahitaji.
Masuala ya kuchezeana faulo za makusudi muda wake umeisha na sasa hakuna vita bali burudani inahitajika uwanjani kwa kila mmoja kufuata maelekezo ya benchi la ufundi.
Mashabiki mnajukumu la kushangilia timu zenu bila kuleta fujo wala kuamini kwamba mtashinda kwani matokeo halisi huwa yanapatikana baada ya dakika 90.
Zile tambo ambazo zinakuwa kwenye mitandao hazipaswi kuwa kwenye uhalisia kwa wakati huu bali kila mmoja awe anaamini kwamba kuna kushinda, kushindwa na sare.
Kila la kheri wachezaji kwenye majukmu yenu ya kila siku tunaamini kwamba itakuwa ni burudani bomba ndani ya dakika 90.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE