Home KITAIFA INJINIA HERSI KAAMUA KUJITUTUMUA NA HILI YANGA

INJINIA HERSI KAAMUA KUJITUTUMUA NA HILI YANGA

0

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Rais wao, Eng. Hersi Said amefunguka kuwa wameweka mikakati ya kuhakikisha wanapata nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Yanga kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar dhidi ya Al Hilal ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 ambapo hofu kubwa ipo kwenye mchezo wa marudiano.

Mchezo wa pili wa marudiano unatarajiwa kupigwa Oktoba 15 mwaka huu kwenye mji wa Khartoum nchini Sudan ambapo Yanga wanapaswa kupata ushindi ili kuvuka hatua hiyo.

Akizungumzia maandalizi yao, Eng. Hersi Said alisema kuwa “Tunajua mashabiki, wapenzi na wanachama wa Yanga kiu yao kubwa ni kuona timu inacheza hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika.

“Hata sisi tunatamani hilo na ndio maana tumewatanguliza watu wetu nchini Sudan ili waweze kuandaa mazingira kwa kushirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini Sudan na kila kitu kinaenda sawa.

“Tunahitaji kuingia kwenye hatua ya makundi na tumejaribu kuongea na wachezaji na benchi la ufundi kwa ajili ya kuhakikisha tunatimiza malengo yetu hivyo tuna imani tutakapoingia kwenye hatua hiyo basi tutafanya tafrija.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here