Jezi aliyoivaa nguli wa soka Diego Maradona katika Fainali za kombe la Dunia mwaka 1986 imerudishwa nchini Argentina.
Mashabiki wa soka nchini humo wamefurahia sana kuiona jezi hiyo ambayo Maradona aliivaa katika kipindi cha pili.
Aliyerudisha jezi hiyo ni nguli wa Ujerumani Lothar Mathaus ambaye katika mchezo huo walibadilishana jezi na Maradona baada ya mechi.
Ameikabidh kwa Chama cha soka cha Argentina.
Katika mchezo huo wa Fainali, Argentina iliifunga Ujerumani.
Shirikisho la Argentina ( AFA) lilimshukuru Mathaus kupitia video.
Mathaus, hata hivyo alisikitika kuirudisha jezi hiyo wakati mhusika mwenyewe Maradona akiwa tayari ametangulia mbele za haki.
Maradona amefariki Dunia mwaka 2020 kwa shinikizo la moyo.
Jezi nyingine ambayo pia Maradona aliivaa katika mchezo wa Robo Fainali wa kombe la Dunia dhidi ya Uingereza ilivunja rekodi ya kuuzwa kwa paundi milioni 7.1 mapema mwaka huu.
Aliyeiuza jezi hiyo ni kiungo wa zamani wa Uingereza Steve Hodge.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE