Home KITAIFA KAMWE AWAVIMBIA WANAOIBEZA YANGA MBELE YA AL HILAL

KAMWE AWAVIMBIA WANAOIBEZA YANGA MBELE YA AL HILAL

0

Ofisa Habari mpya wa Yanga, Ally Kamwe amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo na wapenzi wa soka nchini kuhusu taarifa za baadhi ya wachambuzi wa soka nchini kuwa Yanga haina uwezo wa kuifunga Al Hilal katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Kamwe amesema Ijumaa, Oktoba 30, 2022 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa Yanga inao uwezo wa kuiondoa Al Hilal kutokana na kikosi kilichopo na benchi la ufundi kwani Hilal kwa sasa wanapitia wakati mgumu hata michezo iliyopita dhidi ya St. George walipita kwa bahati.

“Watu wanasema Al hilal wana wachezaji wazuri kisa kuna mchezaji ametoka ASEC Mimosas, Je, hao Al hilal wanajua pia kuwa Eng Hersi alitoa mtu pale ASEC Mimosa? Tena mchezaji bora wa Ligi ya Ivory Coast (Aziz Ki).

“Wanasema Kuna mchezaji katoka As Vita club na wao je kuwa wanajua kuwa Yanga walimsajili mfungaji bora wao na yupo Yanga kwa sasa?

“Wanasema wana mchezaji Kutoka Senegal, Je, jiulize wanajua na sisi tuna mchezaji Kutoka Burundi ambaye kapita EPL tena akitwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Championship?

“Sisi Yanga tuna uwezo wa wachezaji wakubwa kuliko wao na kama pesa na sisi tupo vizuri zaidi yao, tuna Ghalib said Mohamed,” amesema Kamwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here