Home KITAIFA KAZE: MAKAMBO HAMNA KITU SIKU HIZI, TULITAKA MAYELE APUMZIKE TU

KAZE: MAKAMBO HAMNA KITU SIKU HIZI, TULITAKA MAYELE APUMZIKE TU

0

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amekiri mshambuliaji Heritier Makambo alikuwa chini ya kiwango katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold

Hata hivyo Kaze amesema walilazimika kumtumia Makambo ili kumpumzisha Mayele ambaye alipata majeraha wakati wakijiandaa na mchezo dhidi ya KMC

“Ni kweli Makambo hakuwa katika kiwango bora leo lakini ilikuwa ni lazima tumtumie ili kumpa Mayele mapumziko. Mpango ulikuwa kumpa Mayele muda wa kucheza usiozidi dakika 25, anarejea kutoka kwenye majeruhi na tutahitaji kumtumia katika mechi ijayo,” alisema Kaze

Katika mechi mbili dhidi ya KMC na Geita Gold, Makambo amekosa umakini ambapo ameshindwa kutumia nafasi kadhaa za wazi

Makambo alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga, lakini sasa anahitaji kufanya kazi ya ziada katika viwanja vya mazoezi ili kurejea katika ubora wake wa zamani

Ikumbukwe Yanga itaongeza nguvu kwenye dirisha dogo, Yacouba Songne yuko tayari kurejea baada ya kupona majeraha.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here