Wakati Dunia inadhorubika na Kadhia za hapa na pale miaka ya 1940, Alikuwepo Mwanajeshi Mmoja ambaye aliingoza England katika vita vya Pili vya Dunia, Huyu ni Sir Winston Leonard Spencer Churchill Aliyekuwa Waziri Mkuu wa England enzi hizo, yeye ndiye binadamu wa kwanza kurasimishwa akitamka neno “Never Give up”.
Zipo Hotuba nyingi ambazo amewahi kuhutubia, lakini ile ya Oktoba 29 1941 akiwa kwenye vita vya Pili vya Dunia alipowaambia Wanajeshi wa British mara tatu, Never Give up. Never Give Up, Never Give Up, hatimaye Uingereza walimaliza salama Vita hii ya Dunia na wakawepo upande wa Washindi.
Nisikilize Ewe Kibu, wakati unatua Simba Hakuna aliyeamini ungeweza kuperform kwa ukubwa wa aina yake, Hakuna mwalimu aliyekuona Mazoezini na akashindwa kukupa namba timu ya Taifa, Si Pablo Franco wala Si Kim Paulsen, wote walikupa namba tena katika kikosi cha kwanza.
Simba hawakuwa Punguani kupigania Uraia wako, Waliamini, wanaamini na wataamini kwako Mtoto wa mzee Denis Prosper. Imezaliwa Dhamira chafu ya wachache juu yako mwamba, kila ugusapo Mpira safari hii watu wanapunguza imani na makelel yao ya kushangilia wakiamini utaupoteza.
Imani yao inasahau wewe uliwafungia magoli mengi na muhimu msimu uliyopita, wanasahau umelisaidia taifa lako Huru mbele ya makachero wajuaji wa boli, Nisikilize mwamba.
Najua unapitia wakati mgumu kwa sasa, Hasira zinajaza donge zito la Mate ya uchungu kinywani, Nakuomba kaka, Usiyameze mate hayo, utaweka Kinyongo, mashabiki ndivyo tulivyo. Tema mate chini yafukie kisha nenda zako.
Endelea kupiga Kazi Jemedari, endelea kujifua mwamba, Mzingatie mzee Churchill na Hotuba zake, Usikate tamaa, Nyakati njema zinakuja, basi kama ambavyo utamsikiliza Churchill, Msikilize pia Pep Guardiola mnene ukiwa Mo Simba Arena. One day yes kaka.
Form is Temporary but Class is Permanent..
Imeandikwa na Alwatan Adulazeez
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE