Home KITAIFA KIMATAIFA KAZI BADO IPO, MUHIMU KUJITUMA

KIMATAIFA KAZI BADO IPO, MUHIMU KUJITUMA

0

KUPANGA ni kuchagua ikiwa mpango kazi wa kwanza ulikwama basi kuna mpango wa pili ambao huwa na maamuzi ya mwisho kwenye ulimwengu wa mpira.

Kila mmoja kwa sasa macho na maskio ni kwenye mechi za kimataifa ambazo wawakilishi wetu wapo huko wakipambania kombe.

Azam FC wao kazi yao ni dhidi ya Al Akhadar ya Libya baada ya kete ya kwanza ugenini Azam FC kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 na Kipanga wao kazi yao ni dhidi ya Club Africain ya Tunisia baada ya kushindwa kufungana hawa ni kwenye upande wa Kombe la Shirikisho.

Simba wao ni leo kimataifa dhidi ya de Agosto ya Angola ambapo Yanga kete yao ya kwanza ilikuwa dhidi ya  Al Hilal ya Sudan na walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na wanakibarua cha kuwafuata ugenini.

Kwa Simba ambao wataanzia ugenini kazi yao ya pili inatarajiwa kuwa Uwanja wa Mkapa wakiwa nyumbani hapo kazi inabidi kuwa ngumu kwa kila timu.

Imani yetu ni kuona wale ambao walipata matokeo ambayo hawakuhitaji wanapata nguvu ya kwenda kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili ili kusonga mbele.

Kazi ya kupata matokeo kwenye mchezo wa pili huwa inaongezeka ugumu mara mbili iwe upo nyumbani ama ugenini kwa sababu hapo kila timu inasaka hatma yake.

Kutinga hatua ya makundi ni jambo muhimu kwa timu zote ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa kwa kuwa kutafanya bendera ya Tanzania kuzidi kupeperuka kimataifa.

Kugotea kwenye hatua hii ni jambo la huzuni kwa mashabiki na Watanzania wanaopenda michezo hakuna ambaye ataonyesha tabasamu kwenye hili.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here