Home KIMATAIFA KLOPP ALIA NA REFA KIPIGO CHA ARSENAL

KLOPP ALIA NA REFA KIPIGO CHA ARSENAL

0

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemtupia refa ‘zigo la lawama’ kwa kipigo cha magoli 3-2 kutoka kwa Arsenal katika mchezo wa ligi Kuu Uingereza.

Liverpool katika hali ya utata walisababisha penati baada ya Thiago Alcantara alipogongana na Gabriel Jesus ndani ya box ( eneo la penati) na kupelekea Arsenal kupata goli la tatu.

Lakini pia walinyimwa penati baada ya shuti la Diego Jota kugonga mkono wa Gabriel.

Akiongea kuelekea mchezo wao wa leo wa Rangers, Klopp amesema refa bora wa Ligi ya EPL Michael Oliver hakuwa sahihi katika maamuzi yake.

” Kabla ya msimu, tuliambiwa hakuna penati za bure,”

” Lakini cha ajabu tunaziona msimu huu,”

” Tena nyingine za mikono na nyingine kama hizi katika michezo mingine,” amesema.

Hata hivyo, Klopp amekiri Liverpool kufungwa magoli ya kijinga.

” Tumefungwa magoli ya kijinga hasa lile la kwanza katika kipindi cha kwanza,”

Kuelekea mchezo wake na Rangers, amesema Liverpool itasonga mbele ikiwa na mtaji wa magoli 2-0 ya mechi iliyopita.

” Tutafanya vizuri dhidi ya Rangers ,” amesema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here