Home KIMATAIFA KLOPP: TULISHINDWA KUIWEKA MECHI UPANDE WETU

KLOPP: TULISHINDWA KUIWEKA MECHI UPANDE WETU

0

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema safu mbovu ya ulinzi ndio imesababisha kupoteza 2-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Leeds.

Majogoo hao wa Anfield wameangukia katika kipigo cha pili mfululizo baada ya Crysencio Summerville kuachia shuti la kawaida lililokwenda kimiani dakika moja kabla ya refa kumaliza mchezo.

” Ni huzuni kwa kweli,” amesema Klopp.

“Tulisawazisha lakini haikutupa nguvu ya ushindi,”

” Tulipoteza kabisa udhibiti wa mechi,” amesema Klopp.

Mabao ya Leeds jana yalifungwa na Rodrigo dakika ya nne na Crysencio Summerville dakika ya 89, wakati la Liverpool limefungwa na Mohamed Salah dakika ya 14.

Kwa ushindi huo, Leeds wanafikisha pointi 12 katka mchezo wa 12 na kujivuta nafasi ya 15, wakati Liverpool baada ya kichapo hicho cha kwanza nyumbani tangu mwaka 2017, wanabaki na pointi zao 16 za mechi 12 pia nafasi ya tisa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here