Home KITAIFA KMC HAWANA JAMBO DOGO, HIKI WANAKITAFUTA

KMC HAWANA JAMBO DOGO, HIKI WANAKITAFUTA

0

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa unahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulio mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

KMC chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imekusanya pointi 13 baada ya kucheza mechi 8 za ligi, imeshinda tatu, sare nne na imepoteza mchezo mmoja ikiwa nafasi ya tatu.

Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa ubora wa pira kodi, pira mapato unaonekana na kila mpinzani anawahofia.

“Unaona namna ambavyo tunacheza hadi raha, wachezaji wana morali kubwa na wanatimiza majukumu yao malengo yetu ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa ligi kwani ligi bado inaendelea.

“Tumekuwa kipimo sahihi kwa timu zote ambazo zinacheza mechi za kimataifa na tumecheza na Azam FC, Simba nadhani mashabiki waliona namna kazi ilivyokuwa na bado tunazidi kuonyesha ubora wetu,” amesema Mwagala.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here