Home KITAIFA KUHUSU KIWANGO CHA SHOMARY KIBWANA…ZAHERA ASHINDWA KUJIZUIA

KUHUSU KIWANGO CHA SHOMARY KIBWANA…ZAHERA ASHINDWA KUJIZUIA

0

Mkurugenzi wa Soka la Vijana wa Klabu ya Yanga ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema kuwa hata kama yeye angekuwa kocha wa Yanga wakati huu, angekuwa anampa nafasi Kibwana Shomari na Joyce Lomalisa angeendelea kusubiri benchi.


Zahera alisema utofauti wa Kibwana na Lomalisa upo kwenye kukaba, spidi na namna ya kufanya maamuzi kwa wakati. Hivyo Kibwana yupo juu zaidi ya Lomalisa na kwenye kanuni za soka unatakiwa kuanza na mchezaji ambaye ni bora kuliko mwingine.


Zahera alisema kishabiki watu wanaweza wakasema kwamba Lomalisa anayetumia mguu wa kushoto ndiye acheze kama beki namba tatu kuliko Kibwana anayecheza upande wa kushoto wakati kiasilia yeye ni beki wa kulia, mawazo ambayo yapo taofauti na kocha kama yeye.


“Kibwana ni bora zaidi ya Lomalisa, kwa sababu Kibwana na spidi kubwa kwenye kushambulia na kukaba. Lomalisa siyo mbaya lakini hana spidi kwenye kukaba na kushambulia tofauti na Kibwana anavyocheza.
“Kwahiyo maamuzi ya kocha Nabi kuanza na Kibwana kwangu naona ni sahihi sana, hata kama ningekuwa mimi ningeanza na Kibwana hasa kwenye mechi ambazo washambuliaji wake wana nguvu na kasi kubwa,” alisema.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here