Home KITAIFA KUHUSU KIWANGO WA DIARRA SIKU HIZI …..MBRAZILI YANGA AANIKA MBIVU NA MBICHI...

KUHUSU KIWANGO WA DIARRA SIKU HIZI …..MBRAZILI YANGA AANIKA MBIVU NA MBICHI ZOTE

0

Kama ulijua Yanga inamtegemea kipa Mmali, Djigui Diarra pekee kwenye mechi zake za kimashindano basi sahau, kwani kocha wa makipa wa Wanajangwani hao Mbrazil Milton Nienov aweka wazi kila mmoja kwenye eneo hilo ana ubora wa kudaka mechi yeyote.

Licha ya Diarra kuonekana kudaka mechi nyingi za Yanga akifuatia Aboutwalib Msheri huku Eric Johora akionekana kutokuwa na nafasi, Nienov ameweka wazi wote wana ubora wa juu.

Kocha huyo aliyewahi kuinoa Simba kabla ya kujiunga na Yanga msimu uliopita ameeleza kuwa; “Makipa wetu wote wana ubora mkubwa, siwezi kusema wanalingana lakini kila mmoja ana ubora wake, wote wanaweza kucheza mchezo mkubwa wa kimashindano na kufanya vizuri,” alisema Nienov na kuongeza;

“Kinachotokea eneo la kipa sio la kubadili mara kwa mara, na kila mtu anamuda wake ambao ukifika atacheza lakini kiujumla wote wako imara.”

Yanga kwa sasa inajiandaa na mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Hilal itakayopigwa Sudan Oktoba 16, mwaka huu baada ya kutoa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here