Klabu ya Simba Queens imelamba dili la udhamini kutoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet lenye thamani ya shilingi Bilioni 1.
Simba Queens walelamba rasmi dili hilo leo Oktoba 26, 2022 ambapo CEO wa klabu, Barbara ameweka wazi kuwa, mkataba huo ni wa kwanza kwa upande wa timu za wanawake.
“Tulivutana kwa muda mrefu na M Bet mapaka kufikia dili hili. Tuliwashawishi kulingana na thamani ya Simba Queens na mashindano makubwa wanayokwenda kuwakilisha nchi hadi tukafikia hapa.
“Watatoa shilingi milioni mia mbili kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ambapo itawezesha Simba Queens katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo kuonesha live mechi zake kupitia Simba App,” alisema Barbara.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE