Home KITAIFA MANARA AFUNGUKA KUHUSU ALI KAMWE NA PRIVALDINHO

MANARA AFUNGUKA KUHUSU ALI KAMWE NA PRIVALDINHO

0

Hatimaye Haji Manara amefuguka kuhusu kusajiliwa kwa Ali Kamwe kama afisa Habari wa klabu ya Yanga na Privaldinho kama msimamizi wa ‘digital’, Haji Manara amewapongeza na kuwakaribisha vijana hao ndani ya Klabu ya Yanga.

Mbali na kuwapongeza na kuwakaribisha, Haji Manara ameonyesha Imani yake kubwa aliyonayo kwa Ali Kamwe na Privaldinho huku akiahidi kuwaonyesha ushirikiano wa kutosha katika kutimiza majukumu yao katika kuitumikia Klabu ya soka ya Yanga.

“Nawajua ni Vijana Wadogo lakini Very Sharp,Tutawalinda kama wao wanavyopaswa kuilinda hii Club Kwa kila hali.

Tutawasuport na tutawapa dira yetu ya sasa na ya baadae, kikubwa nawasihi Wananchi tuwaunge mkono ili walichonacho kiinufaishe hii Taasisi kubwa zaidi ya kispoti Afrika Mashariki.

Wakati huu nikiwa nje sitaacha kuwapa nilichonacho kwa maslahi ya Club, tumezungumza nao Kwa kina na wanajua Wananchi na Club inategemea nn toka kwao.

Karibuni sana katika Club ya Watu wa Nchi hii, tegemeeni full support yangu binafsi.” Ameandika Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here