BAO la mapema Alex Iwobi ambalo alifunga dakika ya 5 halikutosha kuwapa pointi tatu mbele ya Man Chester United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.
Ni Antony aliweka usawa dakika ya 15 na kufanya ubao wa Uwanja wa Goodison Park kusoma Everton 1-1 United.
Dakika ya 44 Cristiano Ronaldo alipachika bao la ushindi na kuifanya United kwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao 2-1 ambayo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.
United inafikisha pointi 15 ikiwa nafasi ya tano huku Everton ikiwa nafasi ya 12 na pointi 10.
Rekodi zinaoyeshwa kuwa Everton ilipiga mashuti 11 na ni mawili yalilenga lango huku United ikipiga mashuti 12 na manne yalilenga lango
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE