Home KITAIFA MASKINI IHEFU MTIHANI MZITO MBELE GIZA

MASKINI IHEFU MTIHANI MZITO MBELE GIZA

0

Ihefu imesema licha ya kuwakosa nyota wake wanne, lakini kesho inahitaji ushindi wa kwanza baada ya mchezo uliopita kuambulia pointi moja dhidi ya Tanzania Prisons.

Timu hiyo itacheza dhidi ya Mbeya City kesho katika uwanja wa Sokoine, huku rekodi ikiwabeba Ihefu kwani katika mechi mbili za mwisho kukutana kwenye ligi msimu wa 2020/21 ilipata ushindi mmoja na sare ya bao 1-1.

Hata hivyo Ihefu chini ya Kocha wake Mkuu, Juma Mwambusi itakuwa na mtihani mwingine baada ya kucheza mechi tano bila ushindi wowote ikiwa ni vipigo vinne na sare moja, huku City wakishinda moja, sare mbili na kupoteza miwili.

Hadi sasa City wapo nafasi ya 12 kwa alama tano huku Ihefu ikiwa mkiani kwa pointi moja na kesho watakuwa kibaruani kumenyana kuwania alama tatu na kujiweka pazuri.

Kocha Msaidizi wa Ihefu, Themy Felix amesema sare waliyoipata ikiwa ya kwanza kwenye mechi iliyopita imewapa njia rasmi kusaka alama tatu na kwamba wanahitaji kuendeleza rekodi kwa wapinzani hao.

“Benchi la ufundi tumemaliza kazi yetu, tutawakosa wachezaji wanne, Juma Nyosso, Omary Hamis, Joseph Kimwaga na Shaban Kado, lakini wengine wapo fiti na tayari kwa mechi hiyo na tunaamini tutashinda,” alisema Felix.

Kocha Msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima amesema katika mechi mbili za mwisho hawajafanya vizuri lakini wamekuwa na mapungufu kwenye sehemu ya beki, jambo ambalo wamelifanyia kazi.

“Tunaamini kesho tunaenda kufanya vizuri, tutamkosa George Sangija ambaye ana kadi tatu za njano, makosa yaliyoonekana kwenye mechi zilizopita benchi la ufundi limeyafanyia kazi,” amesema Mwamlima.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here