Home KITAIFA MASTAA AZAM KUIFUATA LIBYA, 7 WABAKI

MASTAA AZAM KUIFUATA LIBYA, 7 WABAKI

0

KIKOSI cha wachezaji 25 wa Azam FC wanatarajiwa kukwea pipa kesho Oktoba 6,2022 kuelekea nchini jijini Benghazi, Libya kesho Alhamisi saa 11.25 Alfajiri.

Miongoni mwa mastaa watakaokuwa kwenye msafara huo ni pamoja na kipa namba moja Ali Ahmada,Lusajo Mwaikenda,Bruce Kangwa, James Akaminko.

 Safari hiyo ni kwa ajili ya kwenda kuikabili Al Akhdar ya Libya kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo unatarajia kufanyika Jumamosi saa 2.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.Nyota 7 wanatarajiwa kubaki Bongo kutokana na sababu mbalimbali kama ambavyo imeelezwa na Azam FC namna hii:-
Wilbol Maseke – majeruhi
Kenneth Muguna – majeruhi
Twalib Mohamed – sababu za kiufundi
Ibrahim Ajib – sababu za kiufundi
Ismail Aziz Kader – sababu za kiufundi
Shaaban Idd Chilunda – sababu za kiufundi
Rodgers Kola – sababu za kiufundi

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here