Home KITAIFA MAYELE AWA HABARI YA MJINI TUNISIA, APANGIWA MIKAKATI YA KUCHUNGWA

MAYELE AWA HABARI YA MJINI TUNISIA, APANGIWA MIKAKATI YA KUCHUNGWA

0

KUPITIA maoni (comment) katika ukurasa wa timu ya Club Africain baadhi ya mashabiki wameonesha hofu yao kwa Mshambuliaji huyo kwa kuandika ni mchezaji hatari na wa kuchugwa sana, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza ambao umepangwa kupigwa Jumatano (Novemba 02) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Nguvu ya timu ya Tanzania (Yanga SC) ipo kwa mshambuliaji wa Congo, Kalala Mayele tu. Mshambuliaji huyu anatakiwa kuchugwa sana na akidhibitiwa hakuna hofu kwa klabu yetu ( Club Africain)” ameandika shabiki mmoja wa Club Africain

Mashabiki hao wameendelea kuichambua Young Africans na kusema kuwa ni timu yenye wachezaji bora wenye nguvu na kasi, hivyo sio ya kuidharau kuwa wataifunga kwa urahisi kama ilivyokuwa kwa timu ya Kipanga ya Zanzibar walioifunga bao 7-0.

Fiston Mayele alimaliza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na mabao 7 katika michezo 4. Mabao 6 kati ya hayo alifunga dhidi ya Zalan FC, huku bao moja akilifunga dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here