Home KITAIFA MBEYA CITY WAPINDUA MEZA KIBABE

MBEYA CITY WAPINDUA MEZA KIBABE

0

LICHA ya kupata bao la kuongoza mapema kupitia kwa mzawa Nickosn Kibabage ilikuwa ngumu kwa Mtiwa Sugar kusepa na pointi tatu za Mbeya City.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Manungu Oktoba 2,2022 na bao ulisoma Mtibwa Sugar 2-2 Mbeya City.

Kwa matokeo hayo Mbeya City ni wamepindua meza kibabe.

Bao la mapema kwa Mtibwa Sugar lilijazwa kimiani na Nickson Kibabage dakika ya kwanza, bao la pili likafungwa na Jean Pipi dakika ya 29.

Uongozi wao ulikuwa kwa muda wa dakika 54 kwa kuwa kipindi cha pili mabao yote yaliwekwa usawa.

Ilikuwa dakika ya 55 kwa shuti la Hassan Nassoro kugonga mwamba kumfanya kipa Faroukh Shikalo kwenye harakati za kuokoa mpira ukimgonga kwenye mgongo na kuzama nyavuni.

Bao la pili ni mali ya Tariq Seif dakika 65 na kufanya ubao uwe na usawa.

Sasa Mtibwa Sugar ni nafasi ya 7 pointi 8 na Mbeya City nafasi ya 10 pointi 5 zote zimecheza mechi tano

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here