Home KITAIFA MDAKA MISHALE NA AIR MAULA KIMATAIFA WAMEKIMBIZANA

MDAKA MISHALE NA AIR MAULA KIMATAIFA WAMEKIMBIZANA

0

MDAKA mishale wa Yanga, Djigui Diarra, kwenye anga la kimataifa amekimbizwa na Aishi Manula maarufu Air Manula wa Simba.

Katika mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo Yanga na Simba zimecheza msimu huu, Diarra katunguliwa mabao mawili, huku akiwa na clean sheet mbili.

Alifungwa bao mojamoja dhidi ya Al Hilal nyumbani na ugenini kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Manula akifungwa bao moja dhidi ya Primeiro de Agosto ugenini wakati Simba ikishinda 1-3.

Wote wawili wametoka kukamilisha majukumu ya kimataifa ambapo Yanga imeangukia Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya mtoano, huku Simba ikitinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Leo Jumapili, makipa hao wanatarajiwa kuwa na kazi ya kuonesha pale Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa Kariakoo Dabi kunako Ligi Kuu Bara.

Manula alikosekana katika mchezo wa Ngao ya Jamii wakati Simba ikifungwa mabao 2-1 dhidi ya Yanga, langoni alikaa Beno Kakolanya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here