Home KITAIFA MGUNDA ATAMBA KULIAMSHA ZAIDI MSIMBAZI

MGUNDA ATAMBA KULIAMSHA ZAIDI MSIMBAZI

0

Licha ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Primeiro de Agosto jana jioni, Simba imesema kuwa itajipanga vilivyo katika mechi ya marudiano wiki ijayo ili ipate ushindi utakaowapeleka hatua ya makundi.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya mchezo wa leo dhidi ya Agosto, viongozi wa Simba wamesema kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya katika mechi ya marudiano ili wapinzani wasifanye maajabu ya kuwatupa nje.

“Tunamshukuru Mungu tumepata matokeo mazuri hapa na pongezi nyingi ziende kwa wachezaji na benchi la ufundi.”

“Bado hatujafuzu na tuna mechi ya marudiano hivyo tutajipanga kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu.

Kocha wa Simba, Juma Mgunda alisema kuwa yeye na wachezaji wake hawatobweteka. “Kikubwa tumepata ushindi katika mechi ya kwanza lakini tuna mechi ya pili. Wanasema haijaisha hadi iwe imeisha,” alisema Mgunda.

Meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally aliwataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mechi ya marudiano ili wakamilishe vyema kazi waliyoianza Angola

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here