Home KITAIFA MIEZI MICHACHE BAADA YA KUJIUNGA SINGIDA BIG STARS, WAWA AVUNJA UKIMNYA

MIEZI MICHACHE BAADA YA KUJIUNGA SINGIDA BIG STARS, WAWA AVUNJA UKIMNYA

0

Baada ya timu mpya kwenye Ligi Kuu, Singida Big Stars kuanza kwa kishindo msimu huu, nahodha wake Pascal Wawa amefunguka huo ni mwanzo na malengo yao ni kwenda kimataifa.

Wawa aliyejiunga na Singida mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba baada ya mkataba wake kumalizika ameeleza kwa uzoefu wake wa zaidi ya miaka sita ndani ya Ligi Kuu akiwa na Simba na Azam umemfanya kuielewa ligi hii na analiona chama lake jipya likipiga hatua.

“Singida kwa sasa sio ya kubeza, ina wachezaji wengi wenye ubora na uzoefu wa kutosha ambao wanaweza kuifunga timu yoyote.

“Malengo ni kufanya vizuri kwenye michuano yote ya ndani tutakayoshiriki na kwenda kimataifa msimu ujao jambo ambalo naamini litawezekana,” alisema Wawa anayesifika kwa kuanzisha mashambulizi kwa kupiga pasi ndefu fupi fupi na kuongeza;

“Kuna watu watakuwa wanatuchukulia poa lakini sisi hatujali na mashabiki wetu hawapaswi kuwajibu kwani tunaamini vitendo vitaongea na tutawaziba midomo wengi.” Singida imesajili wachezaji wa kigeni kibao na wengine wa Ligi Kuu ambao wameanza vyema wakishinda mechi mbili, sare mbili na kupoteza moja kati ya tano walizocheza na kukaa nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here