Home KITAIFA MIKOBA YA LAVAGNE MIKONONI MWA ONGALA

MIKOBA YA LAVAGNE MIKONONI MWA ONGALA

0

KALI Ongala kocha wa washambuliaji Azam FC na Agrey Morris kocha mchezaji wamekabidhiwa timu hiyo kwa sasa kuelekea maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.

Ni Dennis Lavagne alikuwa kocha wa timu hiyo wamefikia makubaliano ya kuachana naye kwa kile kilichoelezwa kuwa hajafikia malengo ambayo walikuwa wamekubaliana.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya makocha hao kwa sasa.

“Tumefikia makubaliano ya kuachana na Lavagne kwa kuwa yale ambayo tulifikia naye kwenye makubaliano hayakutimizwa hivyo tumekaa na kufikia makubalinao mazuri.

“Kwa sasa timu ipo chini ya Kali Ongala pamoja na Agrey Moriss ambaye ni kocha mchezaji, tunafanya maandalizi kuelekea mchezo wetu wa ligi dhidi ya Simba ambao wametoka kupata pointi moja dhidi ya Yanga” amesema Ibwe.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 27,2022.

Lavagne aliongoza timu hiyo kwenye mechi 6 ambapo nne zilikuwa za ligi na mbili za Kombe la Shirikisho Afrika, alishinda tatu na kupoteza mechi tatu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here