Home KITAIFA MINZIRO AFUNGUKIA KUPATA POINTI MOJA UGENINI

MINZIRO AFUNGUKIA KUPATA POINTI MOJA UGENINI

0

KOCHA Mkuu wa Geita Gold, Felix Minziro amesema kuwa pointi moja ambayo wameipata ugenini ni muhimu kwao kwa kuwa wanazidi kujiamini kuelekea mechi zijazo.

Ikiwa Uwanja wa Mkwakwani, Geita Gold ilishuhudia ubao ukisoma Coastal Union 0-0 Geita Gold baada ya dakika 90 kukamilika.

Minziro amesema kuwa wanatambua walikuwa wanahitaji pointi tatu muhimu lakini wamepata moja jambo ambalo sio baya.

“Tulikuwa tunahitaji pointi tatu ugenini lakini tumepata pointi moja hiyo sio mbaya kwa kuwa ni pointi muhimu kwetu.

“Kwa matokeo ambayo yametokea tunakwenda kujipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo tunaamini kwamba tutazidi kuwa imara, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema.

Geita Gold inafikisha pointi 7 ikiwa nafasi ya 11 huku Coastal Union inafikisha pointi 8 nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi Kuu  Bara.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here