Home KITAIFA MJAPANI WA GEITA GOLD KILA KITU KIPO POA SASA

MJAPANI WA GEITA GOLD KILA KITU KIPO POA SASA

0

Hizi zinaweza kuwa taarifa nzuri kwa mashabiki wa Geita Gold, baada ya mabosi wa klabu hiyo kufichua kuwa, kiungo wao Mjapan, Shinobu Sakai ‘Shino’ kila kitu kwake kipo freshi na sasa ruksa kuanza kukinukisha kwenye Ligi Kuu Bara akiwa na kikosi hicho.

Mabosi wa Geita wamesema Mjapan huyo wa kwanza kusajiliwa kwenye klabu ya Ligi Kuu Bara, vibali vyake vimepatikana baada ya awali kumkwamisha na sasa ni kazi ya Kocha Fred Felix ‘Minziro’ kumtumia kwenye mechi za Ligi Kuu na Azam Sports Federaion Cup (ASFC).

Kwa taarifa hizo huenda Mjapan akaanza kuonekana uwanjani Oktoba 13 wakati Geita itakapoifuata Coastal Union jijini Tanga, iwapo Kocha Minziro ataamua kumtumia siku hiyo.

Ofisa Habari wa Geita Gold, Samwel Dida alisema Shinobu amepata vibali na sasa anaruhusiwa kuitumikia timu hiyo iliyomsajili kwa ajili ya michuano ya kimataifa kabla tya kutolewa katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Dida alisema changamoto ya vibali vya Shinobu ilitokana kwasababu anatokea nje ya Afrika, hivyo namna ya kupata vibali kutoka Asia ilikuwa ngumu wake lakini wamekamilisha.

“Tumeridhishwa na kiwango chake yuko fiti anaweza kucheza ni kiungo wa chini anakaba anacheza na kuisogeza timu mbele,” alisema Dida na kuongeza;

“Tuna matumaini makubwa akianza kucheza kikosi kitakuwa kizuri lengo letu tunahitaji kuwa na kikosi bora cha ushindani msimu huu kuliko ulivyokuwa msimu uliopita.”

Kuhusu mchezo huo ujao, Dida alisema wanaendelea na maandalizi na benchi la ufundi na wachezaji wanajiweka tayari kwa vita hiyo ya ugenini baada ya kushinda mchezo uliopita jijini Arusha mbele ya wenyeji wao Polisi Tanzania.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here