Home KIMATAIFA MPIRA WA ‘GOLI LA MKONO WA MUNGU’ KUPIGWA MNADA

MPIRA WA ‘GOLI LA MKONO WA MUNGU’ KUPIGWA MNADA

0

Mpira ambao Diego Maradona aliutumia kufunga goli la mkono dhidi ya Uingereza utawekwa sokoni kwa ajili kupigwa mnada.

Mpira huo uliotumika mwaka 1986 kati ya Argentina na Uingereza, unawekwa sokoni kwa dau la kati ya paund milioni 2.5 hadi milioni 3.

Mpira huo unauzwa na aliyekuwa refa wa mchezo huo , Ali bin Nasser, ambaye alilikubali goli hilo la mkono lililofungwa na Maradona, maarufu likijulikana kama ‘ goli la mkono wa Mungu’.

Refa huyo amesema mpira huo ni sehemu ya historia ya mpira wa miguu ulimwenguni.

Mpira huo ulitumika ndani ya dakika 90 zote za mechi hiyo iliyokuwa gumzo duniani kutokana na goli hilo la utata la Maradona.

Maradona aliona isiwe tabu, alifunga goli hilo kwa kuupiga mpira kwa mkono wake na kumfunga kipa wa Uingereza Peter Shilton.

Baada ya kufunga, refa Bin Nasser hakujua kama Maradona ameusukuma mpira huo nyavuni kwa kutumia mkono wake na kulikubali goli hilo.

Baadae katika kulitetea goli hilo, Maradona alidai kuwa alifunga kwa kichwa chake na nguvu kidogo ya mkono wa Mungu ilimsaidia kuusukuma mpira huo nyavuni.

Maradona alionekana shujaa kabla ya kufunga goli hilo baada ya kuwapita wachezaji 5 wa England na mwisho kabisa kumfunga Shilton kwa kutumia mkono wake .

Katika mechi hiyo, Argentina walishinda 2-1 na kushinda kombe la Dunia nchini Mexico.

Mpira huo utauzwa Novemba 16 katika tukio litakaloonyeshwa mubashara ‘ live’ duniani kote.

Wale wote wenye nia ya kuununua mpira huo wanakaribishwa kuwasilisha tenda kuanzia Oktoba 28.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here