Home KITAIFA MWAMUZI WA KADI NYEKUNDU, TUTA, KUAMUA YANGA V SIMBA

MWAMUZI WA KADI NYEKUNDU, TUTA, KUAMUA YANGA V SIMBA

0

WATANI wa jadi Yanga na Simba wapo kwenye mtihani mzito kutokana na kupewa mwamuzi mwenye rekodi ya kutoa kadi za njano, nyekundu pamoja na penalti kwenye mechi ambazo alikuwa kati.

Leo Uwanja wa Mkapa ulimwengu utashuhudia Kariakoo Dabi ambapo tayari waamuzi wameshatangazwa ikiwa ni pamoja na Ramadhan Kayoko atakayekuwa mwamuzi wakati.

Rekodi zinaonyesha kuwa Oktoba 2,2022 wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 3-0 Dodoma Jiji, Kayoko alikuwa mwamuzi wa kati amapo alitoa kadi za njano kwa Mzamiru Yassin dakika ya 86 na Jonas Mkude dakika ya 9

Kwa Dodoma Jiji nyota wao David Kibuta alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 12 na kufanya aweze kutoa jumla ya kadi tatu kwenye mchezo huo ambao ulikuwa wa mwisho kwa Masoud Djuma kukaa kwenye benchi ndani ya Dodoma Jiji.

Agosti 16,2022 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kayoko alikuwa mwamuzi wakati ambapo ubao ulisoma Polisi Tanzania 1-2 Yanga.

Kwenye mchezo huu Kayoko aliwaonyesha kadi ya njano Djuma Shaban dakika ya 49, Heritier Makambo dakika ya 71 alionyeshwa pia kadi ya njano .

Juma Ramadhan alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 10 na Mohamed Mmanga beki wa Polisi Tanzania alionyeshwa kadi mbili za njano dakika ya 44 na 88 na kupelekea kuonyeshwa kadi ya njano.

Pia aliamuru pigo la penalti kwa Yanga dakika ya 11 na mpigaji Fiston Mayele alikwama kufunga baada ya kipa wa Polisi Tanzania Kelvin Igendelezi kuweza kuokoa pigo hilo.

Wengine ambao atafanya nao kazi ya kutafsri shera 17 za mpira ni pamoja na Mohamed Mkono assistance 1,Janeth Balama assistance 2,Elly Sassi 4th huku kamishna wa mchezo akiwa ni Kamwanga Tambwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here