Home KITAIFA PAMOJA NA KUIKOA YANGA JUZI, FEI TOTO AFUNGUKA A-Z ALIYOYAPITIA KABLA YA...

PAMOJA NA KUIKOA YANGA JUZI, FEI TOTO AFUNGUKA A-Z ALIYOYAPITIA KABLA YA MECHI

0

Mfungaji wa goli pekee la Yanga katika mchezo wa juzi dhidi ya KMC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amefichua siri ya kilichomuwezesha kuipa Yanga ushindi kwenye mchezo huo.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo kumalizika katika Dimba la Mkapa kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Feisal aliyefunga bao hilo dakika ya 80 amesema;

“Nilipata hitilafu kidogo tumbo lilikuwa linanisumbua ndiyo maana sikuanza leo (juzi) katika kikosi cha kwanza kwa hiyo nikaanzia nje ili kuona hali yangu kama itakaa sawa.

“Kilichonisaidia kuipa Yanga ushindi nimefuata maelekezo ya mwalimu ambayo alinipatia kabla ya kuingia uwanjani.

“Unajua tumetoka dabi (Simba na Yanga) ni mechi kubwa, kulikuwa na uchovu kwa hiyo mwalimu akaamua kupumzisha baadhi ya wachezaji na wengine walikuwa na majeruhi, wengine hawakuwa fiti, lakini tunamshukuru Mungu tumepata ushindi,” amesema Fei Toto.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here