Home KITAIFA POLISI TANZANIA YAPIGWA DILI ZITO NA NABII…WAPEWA MAJI YA BARAKA KWA AJILI...

POLISI TANZANIA YAPIGWA DILI ZITO NA NABII…WAPEWA MAJI YA BARAKA KWA AJILI YA USHINDI

0

Timu ya mpira wa miguu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC leo imeingia mkataba wa Udhamini wa Maji ya kunywa na Nabii Clear Malisa wa Kanisa la Heaven Of Peace Kingdom Embassy.

Maji hayo aina ya Jordan yatatumika kwa ajili ya Kambi , mazoezini, michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Safarini na Vikao vyote vya timu hiyo.

Mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 50 umesainiwa leo Jumanne (Oktoba 04) Jijini Dodoma, kati ya Nabii Malisa na Katibu Mkuu wa Timu hiyo ASP Michael Mtebene.

Aidha, udhamini huo umejikita katika kuboresha mitandao ya kijamii ya timu kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here