Asalam aleykum Profesa, Tumaini langu u-buheri wa Afya.
Wacha nizime Sigara yangu nisije Banja kama Konde Boy kisha nikutonye ewe shujaa wa Wengi. Lile hekalu la Wakushi pale Madagascar bado halijaisha, wapo wahuni wachache waliyoiba Cement wakapeleka kwao.
Lakini Ule ukuta wa Mzee Magu pale Arusha ulikamilika kwa siku chache tu, Unajua kwanini?
Songa jirani nami nikunong’oneze Mwamba.
Mshairi mmoja kutoka Ireland alipata umaarufu mkubwa sana miaka ya 1980 pale London England, Yote ni kwasababu ya shairi lake la hamasa ya Maisha, aliandika kwamba
“What seems to us as bitter trials are often blessings in disguise.” Jina lake ni Oscar Wilde.
Oscar Alimaanisha kwamba “Kinachoonekana kwetu kuwa majaribu machungu mara nyingi ni baraka zinazojificha.”
Yes Profesa, Unachokipitia kwa sasa ni Majaribu ambayo Yana Baraka mbele yako.
Siyo hadithi tena, Kila kocha wa timu pinzani anayekutana na Wewe hujipanga maradufu.
Hakuna aliyekuja dhidi yako akatoka salama kipindi cha pili kwa ligi ya Hapa Nyumbani, Wewe ni Master sana, Ila unayo mitihani mikubwa ya mbeleni, wa Kwanza ni Jumamosi hii dhidi ya Mtani, wa pili ni dhidi ya ndugu zako Africain.
Ishi nazo vizuri mechi hizo mbili, bila shaka, Ufalme utaendelea kuwa wako, nawajua wananchi wamejawa na upendo kwako, wanakukubali na kukulaki kila uchwao, usiwe na Presha Profesa, Baraka tele zipo Njiani.
Hakuna Dhahabu inayong’aa ambayo haijapita motoni, pengine International games ndiyo moto wako Profesa, Heri na baraka Tele nakutakia, piga Rakaa zako mbili kisha kunywa maji na Energy ya Jembe, hakuna kinachoshindikana.
All the Best Profesa .
.
Ameandika Alwatan Abdulazeez
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE