Home KITAIFA RUNGU LA TFF LATUA AZAM, ZAKAZAKAZI APIGWA FAINI NA KUFUNGIWA

RUNGU LA TFF LATUA AZAM, ZAKAZAKAZI APIGWA FAINI NA KUFUNGIWA

0

Ofisa habari wa Azam FC Thabit Zakaria (Zakazakazi) ametozwa faini ya Tsh 500,000 na kufungiwa kujihusisha na soka katika kipindi cha miezi mitatu.

Thabit amepewa adhabu hiyo kutoka bodi ya Ligi kutokana na kuwashutumu waamuzi wa mchezo wa Azam FC dhidi ya Prisons kupitia mitandao yake kijamii na vyombo vya habari.

Mchezo wa Prisons dhidi ya Azam FC uliyomalizika kwa Azam kupoteza 1-0 ulichezwa katika uwanja wa Sokoine Mbeya.

Aidha, Zakazakazi aliwatolea shutuma waamuzi akisema tangu msimu huu wa ligi uanze, waamuzi wamekuwa wakiinyima haki Azam FC huku akitaja michezo kadhaa ukiwemo pia wa Azam vs Yanga akidai kuwa Azam walinyimwa penati ya wazi.

Thabit pia alidai kuwa Yanga walipewa penati isiyo halali na kuongeza kuwa kuna mpira ulitoka lakini refa hakutoa maamuzi badala yake shambulizi likaendelea na kuzaa bao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here