Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amefikisha mechi 200 akiwa na jezi ya klabu ya KRC Genk ya Ubeligiji, katika mechi hizo amefunga mabao 77 na kutoa asisti 21.
Samatta alijiunga na Genk kwa mara ya kwanza January 29, 2016 akitokea TP Mazembe ya Congo ambapo alitumikia klabu hiyo mpaka 2020 na kutimkia Aston Villa ya England.
Baadae September 20, 2020 alijiunga na Fenebahçe ya Uturuki, August 31, 2021 akajiunga na Royal Antwerp ya Ubeligiji na August 16, 2022 amerejea tena KRC Genk.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE