Home KITAIFA SERENGETI GIRLS ‘WAMKOSHA’ RAIS SAMIA

SERENGETI GIRLS ‘WAMKOSHA’ RAIS SAMIA

0

Rais wa Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na kitendo cha timu ya Taifa ya Wanawake ‘Serengeti Girls’ kutinga hatua ya Robo Fainali ya kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Canada katika michuano hiyo inayoendelea nchini India.

Bao la kusawazisha kwa Tanzania limefungwa na Veronica Mapunda na timu hiyo itakutana na Colombia katika hatua ya robo fainali itakayochezwa Oktoba 22.

Kupitia taarifa yake ya Twitter, Rais Samia amesema amefurahishwa sana na watoto hao kuweka historia ya kufuzu kucheza Robo Fainali ya kombe hilo la Dunia.

“Mmefanya jambo kubwa sana kwa nchi yetu ya Tanzania, nawatakia kila la heri,” ameandika Rais Samia.

Kwa sare hiyo, Serengeti imemaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi D ikiwa na alama 4.

Kabla ya mechi ya jana Oktoba 18, Serengeti Girls waliwafunga Ufaransa 2-1 katika mchezo wa pili kufuatia kipigo cha 4-0 dhidi ya kinara Japan mwenye alama 9.

Katika msimamo wa kundi D, Japan wanaongoza wakiwa na pointi 9 wakifuatiwa na Tanzania yenye pointi 4.

Canada ni watatu wakiwa na pointi 2 huku Ufaransa ikiwa mkiani na pointi moja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here