Ikiwa zimebaki siku mbili kupigwa kwa pambano la mkondo wa pili kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga, Shabiki wa Al Hilal amenunua tiketi ya VIP ya kushuhudia pambano hilo kwa pesa za kitanzania Shilingi milioni 8.
Katika taarifa yake Al Hilal wamemshukuru Shabiki huyo ambae hakutaka jina lake litajwe imeandika;
“Sio jambo jipya kwa mashabiki wa Al Hilal!
Kununuliwa kwa tiketi za mechi yetu ya kwanza dhidi ya Young Africans, mmoja wa mashabiki wetu amenunua tiketi ya VIP kwa thamani ya “Sudan Pound milioni 2” (Tsh. Milioni 8,218,502.03 ) na shabiki huyo hakupendelea kutaja jina lake
Asante kwa mashabiki wetu waaminifu, tunasubiri sapoti na uwepo wenu,”
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE