Home KITAIFA SIMBA LEO KUIKABILI MTIBWA KWA MKAPA

SIMBA LEO KUIKABILI MTIBWA KWA MKAPA

0

Baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye mechi mbili mfululizo, mabingwa wa zamani Simba leo watakuwa na kibarua kingine dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mechi itapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, huku Simba ikiwa na deni kubwa la kulipa kwa mashabiki wake.

Hii ni baada ya kukosa matokeo katika mechi zake mbili zilizopita dhidi ya vigogo Yanga na Azam.

Katika mechi yao dhidi ya mabingwa watetezi Yanga, Simba ililazimishwa sare ya 1-1.

Lakini mbaya zaidi iliangukia katika kipigo kipigo cha 1-0 dhidi ya Wanalambalamba, Azam.

Mtibwa Sugar wanaingia katika mchezo huu wakiwa juu ya Mnyama kwa alama moja lakini wakiwa wamecheza mechi mbili zaidi.

Wakata Miwa hawana rekodi nzuri mbele ya Simba SC baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi tano za Ligi zilizopita, sare mbili vipigo vitatu.

Mtibwa ni ya pili katika msimamo ikiwa na pointi 15 wakati Simba ni ya tatu ikiwa na pointi 14.

Yanga ndio wanaongoza msimamo wakiwa na pointi 20.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here