Home KITAIFA SIMBA WANATOA DARASA KIMATAIFA

SIMBA WANATOA DARASA KIMATAIFA

0

Simba wamefanya kile ambacho wamezoea,Ushindi wa bao kwa bila unawafanya wanatinga hatua ya makundi kwa jumla ya mabao manne kwa moja dhidi ya Primeiro De Agosto.

Mchezo wa leo walicheza kwa utulivu kwa sababu walikuwa na mtaji wa mabao matatu,Primeiro De Agosto walibadilika kidogo wakicheza kwa kukaa nyuma na kuziba hatari,ndio mashuti waliyopiga Simba na kulenga lango yalikuwa mawili kwa dakika zote 90.

Simba anatoa darasa la namna ya mechi za Kimataifa zinavyochezwa hasa faida kutumia uwanja wa nyumbani huku pongezi ziende kwa mashabiki wa Simba ambao leo wamejitokeza kwa wingi dimba la Mkapa.

Jenarali Moses Phiri ana unyumbulifu wa hali juu,akipokea mpira kwa mguu wa kulia ni sawa atakavyopokea kwa mguu wa kushoto anafanya vitu kwa usahihi ule ule. Mgunda ameweka rekodi yake kwa kipindi kifupi ambacho ameongoza Simba hadi sasa.

Katika misimu mitano ya michuano ya Kimataifa yaani Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho,Simba wamecheza makundi mara 4 na robo fainali tatu. Hii si jambo dogo;kwa sasa stori itakuwa kubwa kama watafanikiwa kwenda hatua ya nusu fainali ambayo ndio malengo ya Simba.

Yanga,Azam,Kipanga na wengine kuna darasa Simba wanalitoa Kimataifa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here