Home KITAIFA SIMBA WAPEWA SIRI ZA ‘UCHAWI’ WA FEI TOTO…WAAMBIWA JINSI UNAVYOTUMIKA

SIMBA WAPEWA SIRI ZA ‘UCHAWI’ WA FEI TOTO…WAAMBIWA JINSI UNAVYOTUMIKA

0

Staa wa zamani wa Simba, Yusuph Mgwao amesema Kipa Aishi Manula na mabeki wa timu hiyo wasijikite kuwakaba kina Tusila Kisinda na Fiston Mayele badala yake pia wawe makini na Feisal Salum ‘Fei Toto’ kila anapopata mpira nje ya eneo la hatari na wasipofanya hivyo atawamaliza mapema.

Fei Toto amekuwa mzuri wa kuwafunga makipa wa Ligi Kuu kwa mashuti ya nje ya eneo la hatari ambapo mabao yake mengi anayafunga kwa staili hiyo ambayo mara nyingi mabeki na kipa huishia kuuona mpira ukiwa umetinga wavuni na sasa timu hizo zitakutana leo Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza Mgwao alisema mara nyingi mabeki wanamsahahu sana Fei kila anaposhika mpira badala yake wanawakaba kina Mayele kitu ambacho kinampa nafasi nzuri kiungo huyo kufunga yale mashuti yake.

“Unajua mabeki wengi wanapocheza na Yanga muda mwingi wanakuwa wanadili na Mayele na kina Benard Morrison (ambaye hatacheza) wanamsahau Fei ndio maana anapopata mpira anaweza kufunga yale mabao yake pasipo kudhibitiwa na mabeki,” alisema Mgwao na kuongeza;

“Hivyo sasa mabeki na Manula wanatakiwa kuwa makini kuhakikisha Fei akipata mpira hafanyi kitu chochote wakomae naye asipige kabisa yale mashuti yake wakimsahau basi atawafunga kirahisi tu katika hili pambano.”

Hata hivyo, Mgwao alisema mchezo huo wa Ligi Kuu utakuwa na upinzani mkali kutokana uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa timu hizo mbili na mshindi ni yule atakayekuwa bora zaidi ya mwenzake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here