Home KITAIFA SIMBA YADONDOKA SALAMA ANGOLA SASA KAZI NI MOJA TU

SIMBA YADONDOKA SALAMA ANGOLA SASA KAZI NI MOJA TU

0

Msafara wa Simba umewasili saa 4:30 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Luanda, Angola kwa ndege ya kukodi tayari kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Primero de Agosto.

Mchezo wa awali ya raundi ya kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao, Primiero do Agosto dhidi ya Simba zitavaana kesho Jumapili kwenye Uwanja wa 11 de Novembro.

Ndege hiyo ya shirika la FlightLink iliondoka mnamo saa 10:50 alfajiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Kabla ya kufika Angola, ndege hiyo iliyobeba msafara wa Simba ilitua kwa muda Kigoma kwa ajili ya kujaza mafuta.

Tofauti na ilivyozoeleka nyumbani Tanzania ambako Uwanja wa Julius Nyerere umekuwà na pilikapilika nyingi Uwanja wa Luanda umekuwa tulivu na hauna shughuli nyingi

Hakujawa na usumbufu mkubwa kwa wachezaji, maofisa wa Simba pamoja na watu wengine ambao wameambatana na timu hiyo hapa Angola.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here