Home KIMATAIFA SIMBA YAIBUKA NA USHINDI WA KIBABE UGENINI, 1-3

SIMBA YAIBUKA NA USHINDI WA KIBABE UGENINI, 1-3

0

WAKIWA ugenini leo Oktoba 9,2022 Simba imeshinda kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya de Agosto kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bao la mapema kwa Simba lilifungwa na Clatous Chama dakika ya 8 akitumia pasi ya Agustin Okra.

Bao la pili ni mali ya Israel Mwenda ambaye ni beki alipachika bao hilo dakika ya 62 kipindi cha pili kwa pasi ya Sadio Kanoute.

Ni Moses Phiri yeye alipachika bao la tatu dakika ya 75 akitumia pasi ya Clatous Chama.

Kipindi cha pili de Agosto walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Dago kwa mkwaju wa penalti dakika ya 78 ambao ulimshinda Air Manula.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here