Home KITAIFA SIMBA YAICHAPA 3 : 0 DODOMA JIJI

SIMBA YAICHAPA 3 : 0 DODOMA JIJI

0

Ligi kuu Tanzania bara imeendelea leo ambapo mchezo kati ya Simba na Dodoma Jiji ulipigwa uwanja wa Benjamin mkapa simba ikiwa nyumbani.

Mchezo ulianza mapema tu dakika ya nne Simba ikipata goli la kuongoza, goli la kujifunga kutoka kwa mchezaji wa Dodoma Jiji Abdallah Shaibu ‘Ninja’ katika dakika ya 4.

Katika dakika ya 44 ya mchezo Simba iliongeza goli la pili kupitia mchezaji wao Moses Phiri ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Simba ikimaliza kwa kuongoza 2:0.

Kipindi cha pili kilianza timu zote zikiwa katika hali huku Dodoma Jiji ikibadilika na kuonekana kuwa inatafuta kitu huku safu ya ushambuliaji ya Dodoma Jiji ikionekana kulegalega lakini safu ya ulinzi ikiwa imara.

Dakika ya 85 Habib Kyombo anaindikia goli la tatu Simba ambapo mpaka dakika tisini zinakamilika ubao bado unasoma 3:0.

Matokeo ambayo Simba imeyapata leo yanairejesha tena kileleni katika msimamo wa ligi kuu bara 2022/23.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here