Home KITAIFA SIMBA YAWA ‘KIBOGOYO’ MBELE YA YANGA KWA SIKU 1,345

SIMBA YAWA ‘KIBOGOYO’ MBELE YA YANGA KWA SIKU 1,345

0

BAO la Aziz KI limeisaidia timu yake kuambulia pointi moja baada ya sare ya bao 1-1 huku ikitimia siku 1,345 bila Simba kupata ushindi kwenye Ligi Kuu dhidi ya watani wao.

Mara ya mwisho Simba kupata ushindi mbele ya Yanga Ligi ilikuwa Februari 16, 2019 likikufungwa na Meddie Kagere dakika ya 71 golini akiwa kipa Ramadhan Kabwili.

Mabao yote mawili yalifungwa kipindi cha kwanza Simba wakiwa wa kwanza kupata bao dakika ya 15 kupitia kwa Augstine Okra na bao la Yanga lilifungwa dakika ya 45 kupitia kwa Aziz KI.

Dakika tisini kwenye mchezo huo zimemfanya mwamuzi Ramadhan Kayoko kutoa kadi tisa za njano huku Yanga wakiongoza kwa kuonyeshwa kadi tano na Simba nne.

Kipindi cha pili Yanga waliuanza mchezo kwa kaso dakika 10 zakipindi cha pili baada ya hapo timu zote zilinza kucheza mpira wa kuviziana.

Dakika ya 47 Yanga ilipata kona lakini haikuwa na faida kwao kutokana na kuokolewa na mabeki wa Simba wakiongozw na Joash Onyango ambaye alimnyima zaidi nafasi ya kutetema Fiston Mayele.

Kipindi cha pili kona nne zilichongwa Simba wakipata tatu na zote hazikuwa na madhara langoni mwa waponzani na Yanga walipata moja.

Timu zote zilifanya mabadiliko kwa upande wa Yanga walitoka Jeses Moloko, Kisinda nafasi zao zilichukuliwa na Farid Mussa, Gael Bigirimana na

Kwa upande wa Simba alitoka Sakho, Okra na Mwenda nafasi zao zilichukuliwa na Nyoni, Kyombo na Kibu.

AISHI AOMBA RADHI

Baada ya kipa namba moja wa Simba kuruhusu nyavu zake kutikiswa dakika za mwisho kipa huyo alionekana akiwaomba msamaha mashabiki zake kwa kuweka mkono mmoja kifuani na mwingine juu.

Aishi alifungwa bao la nje ya 18 na Aziz KI kipindi cha kwanza dakika ya 45.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here